Nothing Special   »   [go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Rutherfordi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Rutherfordi (rutherfordium)
Jina la Elementi Rutherfordi (rutherfordium)
Alama Rf
Namba atomia 104
Mfululizo safu Metali ya mpito
Uzani atomia 261.1087
Valensi 2, 8, 18, 32, 32, 10, 2
Densiti 23 g/cm³ (kadirio)
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Asilimia za ganda la dunia 0 % (elementi sintetiki)
Hali maada inaaminiwa ni mango
Mengineyo tamburania, nururifu

Rutherfordi ni elementi sintetiki yenye namba atomia 104 kwenye mfumo radidia, uzani atomia ni takriban 261. Alama yake ni Rf. Jina limechaguliwa kwa heshima ya Ernest Rutherford aliyegundua misingi ya fizikia ya kiini.

Elementi ya kutengenezwa katika maabara

[hariri | hariri chanzo]

Ni elementi sintetiki au tamburania yaani haipatikani kiasili. Sababu yake ni nusumaisha ya isotopi zake ni fupi mno. 265Rf ina nusumaisha ya masaa 13.

Iliripotiwa mara ya kwanza 1964 katika maabara ya taasisi ya utafiti wa kinyuklia huko Dubna (Urusi) ikapewa jina la "kurchatovi". Wataalamu Waamerika walidai baadaye ya kwamba haikuwezekana kurudia majaribio ya Warusi wakaweka ufumbuzi mashakani lakini waliweza kuonyesha njia nyingine jinsi gani kutengeneza eleemti na. 104 wakapendekeza jina Rutherfordi.

Baada ya miaka kadha ya ugomvi juu ya swali hili mapatano yalipatikana kuwa jina ni "Rutherfordi" na elementi iliyofuata na. 105 ikapewa jina Dubni kwa heshima ya maabara ya kirusi.

Jinsi ilivyo na elementi transurania sintetiki kiasi cha elementi kinachotengenezwa ni kidogo mno hivyo hakuna uhakika kuhusu tabia za kikemia. Transurania zote ni nururifu na nusumaisha ya elementi hizi ni fupi mno. Isotopi ya Ruthergordi yenye nusumaisha marefu ina nusumaisha ya masaa 13 tu.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: