Shaba nyeupe
Shaba nyeupe (kwa Kiingereza: brass) ni aloi ya shaba na zinki.
Kiwango cha zinki kinaweza kufikia hadi % 40 lakini hii inaweza kubadilishwa kwa kupata tabia zinazotakiwa.
Rangi ya stani inategemea kiwango cha zinki. Hadi asilimia 20 za stani rangi yake ni kahawia hadi kahawia-nyekundu. Aina hii inaweza kuonekana kama bronzi (shaba nyeusi). Juu ya asilimia 36 za stani huwa njano-nyeupe na kufanana na dhahabu.
Tabia za kimetali zinategemea viwango vya stani pamoja na plumbi na nikeli ambazo zinaungwa pia. Nikeli inaboresha kinga dhidi ya ulikaji.
Matumizi
[hariri | hariri chanzo]Zamani ilikuwa ngumu kiasi kutengeneza shaba nyeupe kwa sababu stani safi haikupatikana kwa urahisi, kwa hiyo kazi ilikuwa ngumu na ghali kiasi. Kwa hiyo katika karne zilizopita ilitumiwa zaidi kwa mapambo na vyombo vilivyotakiwa kuonekana vema bila kuwa na gharama za dhahabu halisi.
Siku hizi kuna matumizi mengi katika teknolojia ya kisasa. Ni kipitishi umeme kizuri lakini imara kuliko shaba tupu. Antena na nyaya za shaba nyeupe zinatumiwa katika vifaa vingi. Shaba nyeupe yenye kiwango cha juu cha stani pamoja na asilimia 1-2 za alumini hufaa kwa beringi.
Ilhali ni nyepesi ya kufulika na hailiki haraka inapendwa kwa kutengeneza ala za musiki kama tarumbeta, tromboni , gunda au saksofoni ambapo husifiwa namna ya sauti inayotokea.
Ramia za bunduki hutengenezwa pia kwa shaba nyeupe.
Katika Afrika ya Magharibi, mafundi na wasanii wa Ufalme wa Benin walitumia bronzi kwa vinyago na sanamu zao na mara kadhaa walichezea aloi hadi kufikia pia shaba nyeupe.
Viungo ya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Brass.org
- Brass Archived 17 Januari 2020 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Shaba nyeupe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |