Nothing Special   »   [go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Tana (ziwa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 21:50, 28 Aprili 2006 na Kipala (majadiliano | michango)
Picha
Ziwa la Tana, picha kutoka angani, 1991
Ziwa la Tana
Jina: Ziwa la Tana
Mahali: Nyanda za juu za Ethiopia, (Afrika ya Mashariki)
Eneo la maji: 2.156 km²
Kina ya chini: 14 m
Mito inayoingia: Rib na Gumara
Mito inayotoka: Abbai (Nile ya buluu)
Uwiano wa maji juu ya UB: 1.788 m
Miji mikubwa ufukoni: Bahir Dar

Ziwa la Tana ni ziwa kubwa la Ethiopia na asili ya Nile ya Buluu. Beseni yake iko taktiban 370 km kaskazini-magharbibi ya Addis Ababa katika nyanda za juu za Ethiopia.

Ziwa la Tana

Umbo la ziwa limebadilika katika karne iliyopita kutokana na mashapo. Kamusi ya mwaka 1888 ilitaja kina ya mita 100, lakini leo ni mita 14 pekee. Eneo la ziwa hubadilika na majira ya mvua au ukame yaani kuwa na maji mengi au kidogo. Mito mingi inaingia ziwani ikiwa mikubwa kati yao ni mito ya Rib na Gumara.

Mto wa Abbai (jina la Kiethiopia la Nile ya buluu) unatoka katika ziwa.

Eneo la Ziwa la Tana ni kitovu cha kihistoria cha Ethiopia ya Kikristo. Katika visiwa vidogo ziwani kuna makanisa na monasteri 20 zilizojengwa tangu karne ya 14 BK.