Nothing Special   »   [go: up one dir, main page]

Zeitgeist (tamka tsait-gaist) ni neno la lugha ya Kijerumani lililopokelewa katika Kiingereza na kutoka hapa kupitishwa kwa lugha mbalimbali kimataifa. Ni muungano wa maneno "Zeit" wakati na Geist roho kwa hiyo maana yake ni "roho ya wakati".

Hutumiwa kutaja mwelekeo wa kiutamaduni, kiakili, kisayansi au kisanii wa watu wengi katika kipindi fulani. [1]

Chimbuko

hariri

Dhana ya zeitgeist ilikuwa maarufu tangu mwanafalsafa Johann Herder Gottfried aliyeitumia kutaja mwelekeo wa kiroho wa karne. Neno lilipokelea na waandishi maarufu kama Schiller na Goethe na kuingia katika lugha za Ulaya.

Mifano

hariri

Kwa mfano baada ya mapinduzi ya Kifaransa 1789 watu wengi katika Ulaya walivutwa na mabadiliko yake wakitafakari hatua za kufanana katika nchi zao. Hapa wengi walisema "zeitgeist" ya kipindi hiki katika Ulaya ilikuwa kimapinduzi. Vivyo hivyo tangu nchi nyingi za Afrika kupata uhuru mnamo 1960 "zeitgeist" katika Afrika ilikuwa ya kujiamini, kujenga taifa na kuwa na matumaini mengi.

Mabadiliko ya fesheni yanayoonekana kwenye mavazi ya watu wakati mwingine ni pia dalili ya aina ya "zeitgeist". Kuna mifano mingi kama vile uenezaji wa blue jeans katika nchi nyingi zilizokuwa zamani suruali ya wafanyakazi ya mikono lakini zilianza kuenea duniani pamoja na muziki wa rock na kuwa ishara ya uhuru wa kibinafsi zikivaliwa na wasanii wengi na siku hizi katika nchi kadhaa hata kwenye mazingira ya ofisini pamoja na watu wengi nje ya kazi.

Magazeti kama vile Guardian.co.uk yana kurasa zinazojadili habari za mielekeo mipya katika muziki, falsafa, fesheni au teknolojia chini ya kichwa "zeitgeist". [2]

Google kila mwaka hutoa orodha ya maneno yanayotafutwa zaidi na watumiaji wake ("most searched keywords annually") chini ya kichwa hiki ca "zeitgeist".[3][4]

Marejeo

hariri
  1. "Zeitgeist". The American Heritage Dictionary of the English Language, Fourth Edition. (2003). 7 Agosti 2009.{{cite web}}: CS1 maint: location (link)
  2. Guardian|date=2011
  3. Google Zeitgist: a year in review or 'what the world searched'
  4. http://www.google.com/intl/en/press/zeitgeist2009/

Viungo vya nje

hariri
Simple English Wiktionary 
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno: