Sataranji
Sataranji (kutoka Kiajemi/Kiarabu شطرنج shatranj; pia: chesi kutoka Kiingereza chess) ni mchezo wa ubao kwa wachezaji wawili.
Ubao wa sataranji
Ubao wa sataranji huwa na umbo la mraba na ndani yake kuna miraba midogo 64 inayobadilishana kwa rangi nyeupe na nyeusi. Kuna pia badiliko la rangi za kahawia nyeupe na kahawia nyeusi au rangi mbalimbali.
Kete za sataranji
Jina la kete | Herufi ya kifupi[1] | Picha |
---|---|---|
Kila mchezaji huwa na kete 16 zinazopangwa kwa namna maalumu ambayo ni sawa kwa kila upande na kila safari. Isipokuwa zinatofautiana kwa rangi, kwa hiyo kuna mchezaji mweupe na mchezaji mweusi. Mweupe huanza mchezo; safari inayofuata wachezaji wanabadilishana rangi.
Kete ni za aina mbili:
- vitunda vinane ambavyo ni kete zenye nguvu ndogo zinasimamishwa kwenye mstari wa pili mbele ya mchezaji. Vitunda vyote ni sawa, hakuna tofauti kati ya kitunda na kitunda.
- kete 8 za juu ambazo ni ngome 2, farasi 2, sataranja 2, malkia 1 na mfalme 1.
Kete za juu zinapangwa kwa namna ifuatayo: ngome -farasi -sataranja -malkia -shaha -sataranja -farasi -ngome.
Mchezo
Mchezo huanzishwa na mchezaji mwenye kete nyeupe anayehamisha kete ya kwanza jinsi anavyoamua. Halafu zamu ya mwenye kete nyeusi hufuata na mchezo unaendelea kwa zamu.
Kila kete ina mwendo wake wa pekee. Kete haiwezi kuhamia mraba wenye kete ya rangi yake. Lakini ikimaliza mwendo wake kwenye mraba wenye kete ya rangi nyingine inaikamata maana yake kuiondoa kutoka ubaoni na kuchukua nafasi yake kwenye mraba. Kete iliyokamatwa hairudi tena: ni kama imefungwa au kufa.
Katika mwendo wake kete haiwezi kupita juu ya miraba yenye kete nyingine isipokuwa kete ya farasi ambayo ina uwezo wa kuruka. Vinginevyo mwendo ama unakwisha mbele ya kete nyingine au inaweza kuikamata na kuchukua nafasi yake.
Shabaha ya mchezo ni ushindi. Ushindi unapatikana kama kete ya shaha inatishwa moja kwa moja na kete nyingine ilhali haina nafasi ya kuhamia mahali pasipo tishio. Shaha haiwezi kukamatwa; ikiweza kushambuliwa bila mahali pa kukimbilia, mchezo unakwisha. Hali hii huitwa kwa lugha nyingi "mat" ambalo ni neno la Kiajemi linalomaanisha "amekwisha, hawezi". Kwa Kiingereza ni "checkmate".
Mwendo
Shaha Shaha ni kete kuu katika mchezo; inatembea hatua 1 (=mraba 1) kila upande. Kuna hatua ya pekee ambayo ni kuruka ngome.
Kitunda
Kete ya Kitunda hutembea mbele bila kunyoka tu hadi mwisho wa ubao. Mwendo wake ni hatua ya mraba mmoja. Lakini hatua yake ya kwanza kama haijatembea bado ina nafasi ya kutembea hatua mbili za mraba. Mara nyingi mchezaji mwenye kete nyeupe huanza mchezo kwa kusukuma kitunda kilichopo mbele ya shaha.
Kitunda kikitembea mbele hakina uwezo wa kukamata kete ya adui iliyopo mbele yake. Kituda hukamata kete iliyopo upande wa kushoto au kulia wa mraba mbele yake.
Kama kitunda kinafikia mstari wa mwisho wa ubao kinaondolewa na kubadilishwa kwa kete nyingine yoyote isipokuwa kete kuu ya shaha. Badiliko la kitunda huwa ni uamuzi wa mchezaji wake.
Sataranji ya posta
Ni aina ya chess ambapo wapinzani huwasilisha mienendo yao kwa kila mmoja kupitia kadi za posta. Hivi sasa barua pepe inatumika. Muda wa mabadiliko unakadiriwa kwa siku na mchezo unaweza kuchukua miezi au miaka kukamilika.
Shirikisko la kimataifa la Mawasiliano la Chess (ICCF) [2] lililoanzishwa mwaka wa 1951, lina jukumu la kuandaa Olimpiki yake na Mashindano ya Dunia.
Mashindano ya Dunia ya ICCF
# | Miaka | Bingwa | Utaifa | |
---|---|---|---|---|
1 | 1950-1953 | Cecil Purdy | Australia | [3] |
2 | 1956-1959 | Viacheslav Ragozin | Urusi | [4] |
3 | 1959-1962 | Alberic O'Kelly | Ubelgiji | [5] |
4 | 1962-1965 | Vladimir Zagorovsky | Urusi | [6] |
5 | 1965-1968 | Hans Berliner | Marekani | [7] |
6 | 1968-1971 | Horst Rittner | Ujerumani | [8] |
7 | 1972-1976 | Jakob Estrin | Urusi | [9] |
8 | 1975-1980 | Jorn Sloth | Denmark | [10] |
9 | 1977-1983 | Tonu Oim | Estonia | [11] |
10 | 1978-1984 | Vytas Palciauskas | Marekani | |
11 | 1983-1989 | Fritz Baumbach | Ujerumani | [12] |
12 | 1984-1991 | Grigory Sanakoev | Urusi | [13] |
13 | 1989-1998 | Mikhail Umansky | Urusi | [14] |
14 | 1994-2000 | Tomu Oim | Estonia | [15] |
15 | 1996-2002 | Gert Timmerman | Uholanzi | [16] |
16 | 1999-2004 | Tunc Hamarat | Austria | [17] |
17 | 2002-2007 | Ivar Bern | Norway | [18] |
18 | 2003-2005 | Joop van Oosterom | Uholanzi | [19] |
19 | 2004-2007 | Christophe Leotard | Ufaransa | [20] |
20 | 2004-2011 | Pertti Lehikoinen | Finland | [21] |
21 | 2005-2008 | Joop van Oosterom | Uholanzi | [22] |
22 | 2007-2010 | Aleksandr Dronov | Urusi | [23] |
23 | 2007-2010 | Ulrich Stephan | Ujerumani | [24] |
24 | 2009-2011 | Marjan Semri | Slovenia | [25] |
25 | 2009-2013 | Fabio Finocchiaro | Italy | [26] |
26 | 2010-2014 | Ron Langeveld | Uholanzi | [27] |
27 | 2011-2014 | Aleksandr Dronov | Urusi | [28] |
28 | 2013-2016 | Leonardo Ljubicic | Kroatia | [29] |
29 | 2015-2018 | Aleksandr Dronov | Urusi | [30] |
30 | 2017-2019 | Andrey Kochemasov | Urusi | [31] |
31 | 2019-2022 | Fabian Stanach Christian Muck Ron Langeveld |
Poland Austria Uholanzi |
[32] |
32 | 2020-2022 | Jon Edwards | Marekani | [33] |
Michezo ya Olimpiki ya ICCF
# | Miaka | Medali ya dhahabu | Medali ya fedha | Medali ya shaba |
---|---|---|---|---|
01. | 1949-1952 | Hungaria | Chekoslovakia | Uswidi |
02. | 1952-1955 | Chekoslovakia | Uswidi | Ujerumani |
03. | 1958-1961 | Muungano ya Sovieti | Hungaria | Yugoslavia |
04. | 1962-1964 | Muungano wa Sovieti | Ujerrumani ya Kidemokrasia | Uswidi |
05. | 1965-1968 | Chekoslovakia | Muungano wa Sovieti | Ujermani Magharibi |
07. | 1972-1976 | Muungano wa Sovieti | Bulgaria | Uingereza |
08. | 1977-1982 | Muungano wa Sovieti | Hungaria | Uingereza |
09. | 1982-1987 | Uingeresa | Ujerumani Magharibi | muungano wa Sovieti |
10. | 1987-1995 | Muungano wa Sovieti | Uingereza | Ujerumani ya kidemokrasia |
11. | 1992-1999 | Chekoslovakia Ujerumani |
Kanada Scotland | |
12. | 1998-2004 | Ujerumani | Lithuania | Latvia |
13. | 2004-2009 | Ujerumani | Czech Republic | Poland |
14. | 2002-2006 | Ujerumani | Lithuania | Marekani |
15. | 2006-2009 | Norway | Ujerumani | Uholanzi |
16. | 2010-2016 | Czech Republic | Ujerumani | Ufaransa |
19050 17. | 2009-2012 | Ujerumani | Hispania | Italy |
18. | 2012-2016 | Ujerumani | Slovenia | Hispania |
19. | 2012-2016 | Bulgaria | Ujerumani | Czech Republic Poland |
20. | 2016-2019 | Ujerumani | Urusi | Hispania |
21. | 2020-2023 | Ujerumani | Luxemburg | Marekani |
Tanbihi
- ↑ Herufi zimetokana na majina ya Kiingereza.
- ↑ ICCF
- ↑ Mashindano ya Dunia-1
- ↑ Mashindano ya Dunia-2
- ↑ Mashindano ya Dunia-3
- ↑ Mashindano ya Dunia-4
- ↑ Mashindano ya Dunia-5
- ↑ Mashindano ya Dunia-6
- ↑ Mashindano ya Dunia-7
- ↑ Mashindano ya Dunia-8
- ↑ Mashindano ya Dunia-9
- ↑ Mashindano ya Dunia-11
- ↑ Mashindano ya Dunia-12
- ↑ Mashindano ya Dunia-13
- ↑ Mashindano ya Dunia-14
- ↑ Mashindano ya Dunia-15
- ↑ Mashindano ya Dunia-16
- ↑ Mashindano ya Dunia-17
- ↑ Mashindano ya Dunia-18
- ↑ Mashindano ya Dunia-19
- ↑ Mashindano ya Dunia-20
- ↑ Mashindano ya Dunia-21
- ↑ Mashindano ya Dunia-22
- ↑ Mashindano ya Dunia-23
- ↑ Mashindano ya Dunia-24
- ↑ Mashindano ya Dunia-25
- ↑ Mashindano ya Dubia-26
- ↑ Mashindano ya Dunia-27
- ↑ Mashindano ya Dunia-28
- ↑ Mashindano ya Dunia-29
- ↑ Mashindano ya Dunia-30
- ↑ Mashindano ya Dunia-31
- ↑ Mashindano ya Dunia-32
Viungo vya Nje
- ChessFish Portal Archived 10 Mei 2008 at the Wayback Machine.
- RSS Chess Feeds Archived 8 Julai 2011 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Sataranji kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |