Nothing Special   »   [go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Wilaya ya Marakwet

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wilaya ya Marakwet ilikuwa wilaya mojawapo ya Mkoa wa Bonde la Ufa wa Jamhuri ya Kenya hadi ilipopitishwa katiba mpya ya nchi (2010).

Makao makuu yalikuwa mjini Kapsowar.

Kwa sasa imekuwa sehemu ya kaunti ya Elgeyo-Marakwet.

Wilaya hii ilikuwa na jumla ya wakazi 140,629 [1]. Wakaazi wenyeji ni haswa wa kabila la Wamarakwet.

Wilaya hii iliundwa mwaka wa 1927 kama Elgeyo/Marakwet District. Iligawanywa mara mbili na kuunda Wilaya ya Keiyo na Marakwet mwaka wa 1994.

Wakimbiaji wengi mashuhuri Wakenya hutoka Marakwet, na wanaojulikana ni pamoja na Moses Kiptanui, Evans Rutto, Reuben Kosgei, Ezekiel Kemboi na Richard Chelimo.

Wilaya hii ilikuwa na serikali ya mtaa moja tu, Baraza la Mji wa Marakwet. Kwa hiyo, idadi yake ya watu ni sawa na idadi ya wilaya (140,629). Baraza na Wilaya haina idadi ya wakaazi wanaotambulika kama wakaazi wa mjini (sensa ya 1999) [2].

Maeneo ya utawala

[hariri | hariri chanzo]
Tarafa Idadi ya Watu Makao makuu
Chebiemit 18,559 Chebiemit
Kapcherop 39,328 Kapsowar
Kapsowar 19,647 Kapsowar
Kapyego 11,452 Kapyego
Tirap 23,311 Kapchebau
Tot 17,744 Tot
Tunyo 10,588

Maeneo Bunge

[hariri | hariri chanzo]

Eneo la wilaya hii lina maeneo bunge mawili:

  1. Communications Commission of Kenya: Status of Coverage of Communications Services Archived 28 Septemba 2007 at the Wayback Machine.
  2. Kenya National Bureau of Statistics: Population of local authorities Archived 28 Septemba 2007 at the Wayback Machine.