Peter Debye
Mandhari
Peter Joseph William Debye (24 Machi 1884 – 2 Novemba 1966) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Uholanzi. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Petrus Josephus Wilhelmus Debije. Baadhi ya utafiti mwingine alichunguza mfumo wa atomu, mionzi ya eksirei, na sifa za gesi. Mwaka wa 1936 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia. Mwaka wa 1940, kabla WaNazi hawajavamia Uholanzi, Debye alihamia Marekani alikoishi hadi kifo chake.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Peter Debye kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |