Siku tatu kuu za Pasaka
Mandhari
Mwaka wa liturujia |
---|
Magharibi |
Mashariki |
Siku tatu kuu za Pasaka ndizo kiini cha mwaka wa Kanisa.
Zimekusudiwa kumuadhimisha Yesu mteswa, mzikwa na mfufuka, yaani:
- siku ya kwanza (Alhamisi kuu jioni hadi Ijumaa kuu jioni) inaadhimisha mateso yake kuanzia karamu ya mwisho hadi kifo chake juu ya msalaba;
- siku ya pili (Ijumaa kuu jioni hadi Jumamosi kuu jioni) inaadhimisha maiti yake kubaki kaburini na roho yake kushukia kuzimu;
- siku ya tatu (kuanzia Jumamosi kuu jioni hadi Jumapili ya Pasaka jioni) inaadhimisha ufufuko wake mtukufu.
Siku hizo tatu ni kama bawaba kati ya Kwaresima na kipindi cha Pasaka. Ingawa tarehe zinabadilika kila mwaka, zinaangukia daima kati ya Machi mwishoni na Aprili mwishoni.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Eighteen Questions on the Paschal Triduum Archived 8 Agosti 2011 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Siku tatu kuu za Pasaka kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |