Satiro wa Milano
Satiro wa Milano (Trier, leo nchini Ujerumani, au Roma, Italia, 330 hivi - Milano, Italia, 378), alikuwa kaka wa Ambrosi ambaye alipendana naye kwa dhati na alitaja stahili zake.
Huyo mdogo wake alipochaguliwa kuwa askofu wa Milano, Satiro aliacha cheo chake cha gavana akamsaidie yeye na dada yao Marselina aliyeamua kushika ubikira wake kwa ajili ya Mungu.
Ingawa alikuwa hajaingizwa katika mafumbo ya Kristo, alipovunjikiwa meli baharini, hakuogopa kifo, lakini, ili asife kabla hajapokea sakramenti, aliponusurika alijiunga na Kanisa la Mungu.
Kidogo kabla ya kufariki dunia alipata ubatizo na baada ya kufa mdogo wake alitangaza sifa zake na kumzika karibu na Vikta Mwafrika [1].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 17 Septemba[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |