Nothing Special   »   [go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Nyama choma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyama choma hotelini.
Nyama choma kwenye jiko dogo la makaa.

Nyama choma ni nyama iliyopikwa kwa kuchomwa kwa moto, makaa au jiko la umeme. Pia nyama inaweza kuchomwa na majiko maalum ya kisasa ya gesi ya kuchomea nyama.

Nyama inaweza ama kuchomwa moja kwa moja, ama kwanza kuchemshwa au kupikwa na moshi, mtindo maarufu hasa Marekani, kabla ya kuchomwa.

Harufu yake inavutia watu wengi kuipenda katika nchi na tamaduni mbalimbali duniani. Hivyo imekuwa biashara hasa katika barabara za mijini.

Nyama hii hupendwa pia wakati wa sherehe, matukio muhimu ya kifamilia na marafiki au mwisho wa wiki kwa wale wanaokunywa pombe. Pamoja na kuliwa na vyakula vingine, mara nyingi huandaliwa na kachumbari.

Tofauti za nyama choma duniani

Afrika ya Mashariki

Nyama choma ni maarufu sana Afrika Mashariki, hasa Tanzania na Kenya. Nyama choma katika nchi hizi huitwa mishikaki.

Afrika Kusini

Huko Afrika Kusini nyama huitwa braai kutokana na neno la Kiafrikana "braaivleis."

Namibia

Nchini Namibia, nyama choma ambayo huitwa kapana huchomwa kwa moto wa kuni. Nyama hii hukatwa vipande vidogo na kuchomwa sio zaidi ya dakika 10. Ni nyama maarufu sana kwenye masoko na sehemu za starehe.

Uswidi

Nchini Uswidi, kuchoma nyama moja kwa moja kwenye makaa ya moto ndio njia maarufu.

Mexico

Mexican carne asada. Nyama choma aina ya Chorizos.

Kaskazini mwa Mexico, carne asada ni chakula kikuu. Aina maarufu ni pamoja na arrachera, beefsteak na rib eye, pamoja na chorizo. Kuni na makaa hutumiwa.[1]

Argentina na Uruguay

Huko Argentina na Uruguay, asado (nyama iliyochomwa kwenye moto wa wazi) na a la parrilla (nyama ya ng'ombe iliyochomwa kwenye jiko la asili) ni moja ya chakula kikuu.

Japani

Jiko la kiasili la kuchoma nyama nchini Japani liitwalo "Shichirin"

Kwenye miji ya nchini Japani, mikokoteni ya yakitori, migahawa au madukani, nyama chomwa huuzwa. Nyama iliyolainishwa kwa marinadi huchomwa kwenye jiko la mkaa kwa kutumia vijiti. Huko Malaysia, Singapore, Indonesia, na Thailand, nyama choma iitwayo satay, ambayo ni nyama iliyolainishwa na kuchomwa kwa makaa kisha huliwa na karangawhich is marinated meat on a bamboo skewer grilled over a charcoal fire and served with peanut (sate) sauce.

Athari za kiafya

Utafiti unaonyesha kuwa kuchoma nyama kwa joto la juu kunaweza kusababisha magonjwa mbalimbali.[2][3] Lakini kulainisha nyama kwa kutumia marinadi kunaweza kupunguza hatari ya magonjwa hayo.[4]

Nyama chooma huaminika kuwa njia mbadala bora ya kupika kuliko kutumia mafuta, ingawa uchomaji unaweza kufanya nyama kuwa kavu.[5]

Marejeo

  1. "Weekends have a carne asada smell to them". Mexico News Network. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-20. Iliwekwa mnamo 12 Julai 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Sugimura, Takashi; Wakabayashi, Keiji; Nakagama, Hitoshi; Nagao, Minako (Aprili 2004). "Heterocyclic amines: Mutagens/carcinogens produced during cooking of meat and fish". Cancer Science. 95 (4): 290–299. doi:10.1111/j.1349-7006.2004.tb03205.x. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Juni 2010. Iliwekwa mnamo 1 Februari 2015. {{cite journal}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Chemicals in Meat Cooked at High Temperatures and Cancer Risk - National Cancer Institute". Cancer.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-12-21. Iliwekwa mnamo 2015-02-01. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
  4. "Health | Marinating 'may cut cancer risk'", BBC News, 2008-12-30. Retrieved on 2015-02-01. Archived from the original on 2008-12-31. 
  5. Beckett, Fiona (2012). Sausage & Mash (kwa Kiingereza). London: Bloomsbury Publishing. uk. 16. ISBN 9781408187760. Iliwekwa mnamo 10 Februari 2017.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyama choma kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.