Nothing Special   »   [go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

New York

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mji wa New York


Jiji la New York City
Jiji la New York City is located in Marekani
Jiji la New York City
Jiji la New York City

Mahali pa mji wa New York City katika Marekani

Majiranukta: 40°42′15″N 73°55′5″W / 40.70417°N 73.91806°W / 40.70417; -73.91806
Nchi Marekani
Jimbo New York
Wilaya New York
Kings
Queens
Bronx
Richmond
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 8,336,697
Tovuti:  www.nyc.gov
Majengo marefu ya kisiwa cha Manhattan katika mji wa New York City

New York (Kiing.: "New York City") ni jiji kubwa kabisa Marekani na kati ya miji mikubwa duniani. Iko kwenye pwani la kaskazini-mashariki ya Marekani katika jimbo la New York.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Mji uko kwenye mdomo wa pamoja ya mito Hudson na East River inapoishia katika Atlantiki kwa 40°42N 74°00W.

Kitovu cha mji kipo kwenye kisiwa cha Manhattan kilichopo kati ya Hudson na East River. Eneo la jiji ni funguvisiwa kwenye mdomo huo na visiwa vyake pamoja na Manhattan ni Staten Island, Long Island na visiwa vingine vidogo kwa mfano kisiwa cha Ellis na kisiwa cha Sanamu ya Uhuru (statue of liberty).

Jiji limepanuka kutoka kando za mito hadi barani. Eneo lote la jii ni kilomita za mraba 831.4.

Ndani ya jiji kuna mitaa au wilaya tano zinazoitwa boroughs ambazo ni:

Historia

[hariri | hariri chanzo]
Peter Stuyvesant alikuwa gavana wa mwisho wa Uholanzi wa Nieuw Amsterdam

Jina la Manhattan lakumbuka wakazi asilia waliokuwa Maindio wa Lenape na "manhattan" ni neno la lugha yao "Manna-hata" lililomaaanish a "kisiwa cha milima mingi". Mzugu wa kwanza aliyefika alikuwa nahodha Mwitalia Giovanni da Verrazano mwaka 1524 halafu Mwingereza Henry Hudson mwaka 1609.

Mji mwenyewe ulianzishwa na Waholanzi kwa jina la "Nieuw Amsterdam" (Amsterdam Mpya). Mwaka 1626 kisiwa cha Manhattan kilinunuliwa kwa 60 gulder kutoka wenyeji kikawa mji mkuu wa koloni ya Nieuw Nederland (Uholanzi Mpya).

Mwaka 1664 baada ya vita kati ya Uholanzi na Uingereza koloni yote ilihamishwa upande wa Uingereza pamoja na mji mwenyewe ikapewa jina jipya la "New York".

Katika karne ya 18 New York ilikuwa sehemu ya uasi dhidi ya Uingereza

Kipindi kikubwa cha mji kulitokea katika karne ya 19 wakati wahamiaji wengi sana walipofika MArekani. Idadi kubwa walifika kwenye bandari la New York.

Baada ya fitina kati ya watu wa kusini na wenyeji wa kaskazini serikali ya Kiingereza ilifunga kambi hilo.

Hali ya hewa

[hariri | hariri chanzo]
Viwango vya juu na chini vya joto katika miji ya New York[1] (Fahrenheit)
Jiji  Jan   Feb   Mar    Apr   Mei   Jun   Jul   Aug   Sep   Oct   Nov   Dec 
Albany juu
chini
31
13
34
16
44
25
57
36
70
46
78
55
82
60
80
58
71
50
60
39
48
31
36
20
Binghamton juu
chini
28
15
31
17
41
25
53
35
66
46
73
54
78
59
76
57
68
50
57
40
44
31
33
21
Buffalo juu
chini
31
18
33
19
42
26
54
36
66
48
75
57
80
62
78
60
70
53
59
43
47
34
36
24
Long Island juu
chini
39
23
40
24
48
31
58
40
69
49
77
60
83
66
82
64
75
57
64
45
54
36
44
28
New York City juu
chini
38
26
41
28
50
35
61
44
71
54
79
63
84
69
82
68
75
60
64
50
53
41
43
32
Rochester juu
chini
31
17
33
17
43
25
55
35
68
46
77
55
81
60
79
59
71
51
60
41
47
33
36
23
Syracuse juu
chini
31
14
34
16
43
24
56
35
68
46
77
55
82
60
80
59
71
51
60
40
47
32
36
21
  1. "Typical High and Low Temperatures For Various New York Cities". US Travel Weather. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-03-13. Iliwekwa mnamo 24 Machi 2010.



Majimbo na maeneo ya Marekani
Majimbo ya Marekani
AlabamaAlaskaArizonaArkansasCaliforniaColoradoConnecticutDelawareFloridaGeorgiaHawaiiIdahoIllinoisIndianaIowaKansasKentuckyLouisianaMaineMarylandMassachusettsMichiganMinnesotaMississippiMissouriMontanaNebraskaNevadaNew HampshireNew JerseyNew MexicoNew YorkNorth CarolinaNorth DakotaOhioOklahomaOregonPennsylvaniaRhode IslandSouth CarolinaSouth DakotaTennesseeTexasUtahVermontVirginiaWashingtonWest VirginiaWisconsinWyoming
Mkoa wa Mji Mkuu
Mkoa wa Columbia (Washington D.C.)
Visiwa vya ng'ambo
Katika Pasifiki: Samoa ya MarekaniVisiwa vya Mariana ya KaskaziniGuamKatika Karibi: Puerto RicoVisiwa vya Virgin vya MarekaniVisiwa vidogo sana vya Pasifiki:Kisiwa cha HowlandKisiwa cha Jarvis Atolli ya JohnstonKingman ReefAtolli ya MidwayKisiwa cha BakerAtolli ya PalmyraKisiwa cha WakeKisiwa kidogo cha Karibi: Kisiwa cha Navassa