Nothing Special   »   [go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Mwamba mashapo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Aina mbili za mwamba mashapo: chini mwambatope, juu gange. Plateau Plateau, Tennessee, Marekani.
Jiwe mchanga jekundu linaonyesha tabaka jinsi mchanga wake ulivyokaa.
Kuunganishwa kwa punje za mchanga zikiathiriwa na shinikizo kubwa sana. Pale punje zinapogusana shinikizo kuu linasababisha kuyeyuka kwa mata inayoanza kujaza nafasi kati ya punje. Punje zilizogusana zinaunganishwa kwa njia hii na nafasi zinapungua. Kadri shinikizo linaendelea kwa muda mrefu, mwaba huwa mgumu zaidi na kuongeza densiti. Kwa njia hii mchanga unaweza kubadilika kuwa jiwe mchanga.

Miamba mashapo (kwa Kiingereza: sedimentary rocks) hutokea pale ambapo mashapo hukaa kwa muda mrefu yakifunikwa na mashapo mengine na kuathiriwa na uzito wa matabaka ya juu yanayosababisha shinikizo kubwa. Miamba ya aina hiyo hufanya sehemu kubwa ya uso wa ardhi, ingawa Dunia kwa jumla kuna zaidi miamba ya mgando (igneous rocks) na miamba metamofia (metamorphic rocks).

Asili ya miamba mashapo

[hariri | hariri chanzo]

Mashapo kwa kawaida ni mata inayokusanyika chini kwenye mito, maziwa na bahari baada ya kupelekwa huko na mwendo wa maji, kiasi pia kwa mwendo wa upepo. Mata ya mashapo ni pamoja na vipande vidogo vya mawe yaliyosagwa au kuvunjikavuunjika, mabaki ya mimea au wanyama na mata yaliyotokana na utendanaji wa kikemia.

Aina za miamba mashapo

[hariri | hariri chanzo]

Miamba mashapo inapatikana hasa ya aina tatu: gange (mawe ya chokaa, limestone), jiwe mchanga (sandstone) na mwambatope (shale). [1]

Miamba mashapo hufunika asilimia 75  – 80 za uso wa ardhi, lakini hufanya 5% tu za ganda la Dunia. Viwango husianifu wa aina za miamba mashapo ni kama ifuatavyo:

  • Mwambatope ---------- 60%
  • Jiwe la mchanga-- 20%
  • Gange (CaCO3) --- 15%
  • Mengine ----- 5%

Kuimarishwa

[hariri | hariri chanzo]

Kama mashapo yameshinikizwa kwa nguvu ya kutosha kwa muda mrefu, huimarishwa na kugeuka kuwa mwamba thabiti. Iliyopandwa na kushinikizwa kwa muda, matope huwa 'yameunganishwa' (yamefanywa kuwa thabiti) kuwa safu ya mwamba. Katika mwamba huo matabaka yanatambulika yanayoonyesha jinsi gani mashapo yalivyojipanga wakati wa kushuka kwenye tako la bahari na kufunikwa na matabaka mapya.

  1. Blatt H; Middleton G. & Murray R. 1980. Origin of sedimentary rocks. Prentice-Hall.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwamba mashapo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.