Nothing Special   »   [go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Kyriakos Mitsotakis

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kyriakos Mitsotakis

Mitsotakis in 2021

Waziri mkuu wa Ugiriki
Rais Prokopis Pavlopoulos
Katerina Sakellaropoulou

signature

Kyriakos Mitsotakis (kwa Kigiriki: Κυριάκος Μητσοτάκης; alizaliwa 4 Machi 1968) ni mwanasiasa wa Ugiriki ambaye alihudumu kama waziri mkuu wa Ugiriki tangu mwaka 2019. Tangu mwaka 2016 ndiye mwenyekiti wa chama cha Nea Demokratia (Demokrasia Mpya). Hapo awali alikuwa kiongozi wa upinzani katika bunge la Ugiriki kati ya 2016 na 2019.

Alitangulia kuhudumu kama Waziri wa Marekebisho ya Utawala kati ya 2013 na 2015.

Mitsotakis alichaguliwa kwa mara ya kwanza katika bunge la kitaifa kwa eneo la Athens B mnamo mwaka 2004. Baada ya chama chake cha Nea Demokratia kushindwa katika chaguzi mbili mnamo mwaka 2015, alichaguliwa kuwa kiongozi wa chama hicho mnamo Januari 2016[1]. Miaka mitatu baadaye, aliongoza chama chake katika ushindi wa uchaguzi wa kitaifa mwaka 2019 [2].

  1. Free-market reformer Mitsotakis wins vote to lead Greece opposition party, Hope, Kerin (10 January 2016) kwenye gazeti la Financial Times ya tarehe 10.01.2016, iliangaliwa Juni 2022
  2. Conservative leader Mitsotakis becomes Greek PM, picks cabinet Archived 8 Julai 2019 at the Wayback Machine., Reuters News ya 8 Julai 2019, gazeti la Cyprus Mail, iliangaliwa Juni 2022)