Karne ya 14
Lango la Historia | Lango la Biografia | Karibuni | Orodha ya Miaka
◄ |
Karne ya 12 |
Karne ya 13 |
Karne ya 14
| Karne ya 15
| Karne ya 16
| ►
Miaka ya 1300 |
Miaka ya 1310 |
Miaka ya 1320 |
Miaka ya 1330 |
Miaka ya 1340 |
Miaka ya 1350 |
Miaka ya 1360 |
Miaka ya 1370 |
Miaka ya 1380 |
Miaka ya 1390
Karne ya 14 ilikuwa kipindi cha miaka mia moja kati ya 1301 hadi 1400. Kikamilifu kilianza tar. 1 Januari 1301 na kuishia 31 Desemba 1400. Namba zake zinafuata hesabu ya miaka "baada ya Kristo".
Kama kila "karne" ni kipindi kinachohesabiwa kwa hiari ya kibinadamu kwa sababu ni mgawanyo wa kalenda tu - hali halisi maendeleo na mabadiiliko makubwa hayafuati migawanyo ya kalenda ya kibinadamu.
Kuna mambo mengi yaliyotokea wakati wa karne hii.
Watu na matukio
[hariri | hariri chanzo]Karne ya saa za kwanza
[hariri | hariri chanzo]Labda badiliko kubwa lilikuwa uenezi wa saa za kimekanika kwenye minara ya miji ya Ulaya. Tofauti na saa za jua au saa za maji ziliwaonyesha watu wengi wakati tena bila ya kutegemea hali ya hewa. Wataalamu wengi huamini ya kwamba hakuna mitambo mingine iliyobadilisha utamaduni wa binadamu kuliko saa.
Karne ya kifo katika Ulaya
[hariri | hariri chanzo]Ulaya iliathiriwa mara ya kwanza na ugonjwa wa kuambukiza wa tauni. Tauni iliua wakulima wengi ikasababisha njaa kali; zote pamoja zikaua zaidi ya theluthi ya wakazi wote wa Ulaya. Vifo vingi vilisababisha hofu kubwa kati ya watu. Wayahudi walishtakiwa kuwa sababu ya maradhi na vifo wakauawa na kudhulumiwa katika nchi nyingi za Ulaya.
Uenezaji wa milki ya Waturuki Waosmani
[hariri | hariri chanzo]Udhaifu wa Ulaya katika karne hii ilisaidia uenezaji wa milki ya Waturuki Waosmani kutoka Anatolia kujiandaa kuingia nchi za Balkani (Ulaya ya Kusini-Mashariki). Hivyo utawala wa Kiislamu ulielekea kuenea hata katika mashariki ya Ulaya utakaokuwepo kwa karne tano zilizofuata. Baadaye athira yake ilifikia pwani za Uswahilini na Uganda.
Milki za Afrika
[hariri | hariri chanzo]Katika Afrika ya Magharibi Wahaussa wanaunda milki zao za kwanza. Mali inapanuka. Majengo makubwa ya Zimbabwe Kuu yanaanzishwa.