Kalimantan
Kalimantan (inajulikana pia kwa jina la Borneo ya Indonesia) ni sehemu kubwa ya kisiwa cha Borneo iliyopo Indonesia.[1] Sehemu hii ni asilimia 73 za eneo lote la kisiwa hicho. Sehemu nyingine zisizo za Indonesia ni Brunei na Malaysia ya Mashariki.
Etimolojia
[hariri | hariri chanzo]Jina la Kalimantan (pia Klemantan) linatokana na lugha ya {{Kisanskrit]]: Kalamanthana ikimaanisha kisiwa chenye hali ya hewa joto sana. Linafanywa na maneno mawili: kal(a) (wakati. majira) na manthan(a) (moto sana, ya kuchoma). [2]
Eneo
[hariri | hariri chanzo]Sehemu hii ya Indonesia ina asilimia 73 (km² 544,150 [3]) za kisiwa chote cha Borneo na 69.5% (watu 13,772,543 wakati wa sensa ya 2010) za wakazi wa kisiwa hiki. Sehemu zisizo za Kiindonesia ni Brunei (wakazi 400,000) na Malaysia ya Mashariki (wakazi 5,625,000) inayokumlisha majimbo ya Sabah, Sarawak na eneo la Labuan.
Utawala
[hariri | hariri chanzo]Kalimantan ina mikoa 5 :
Mkoa | Eneo(km2) | Wakazi (2005C) | Wakazi (2010C) | Wakazi (2015C prelim) | Watu/km2 | Makao makuu ya mkoa | Mji mkubwa |
---|---|---|---|---|---|---|---|
West Kalimantan (Kalimantan Barat) |
147,307.00 | 4,042,817 | 4,393,239 | 4,783,209 | 32.5 | Pontianak | Pontianak |
Central Kalimantan (Kalimantan Tengah) |
153,564.50 | 1,913,026 | 2,202,599 | 2,490,178 | 16.2 | Palangkaraya | Palangkaraya |
South Kalimantan (Kalimantan Selatan) |
38,744.23 | 3,271,413 | 3,626,119 | 3,984,315 | 102.8 | Banjarmasin | Banjarmasin |
East Kalimantan (Kalimantan Timur) |
129,067 | 2,840,874 | 3,550,586 | 3,422,676* | 26.5 | Samarinda | Samarinda |
North Kalimantan (Kalimantan Utara) |
71,176.72 | 473,424 | 524,526 | 639,639 | 8.5 | Tanjung Selor | Tarakan |
Total | 544,150.07 | 12,541,554 | 14,297,069 | 15,320,017 | 28 | - | Banjarmasin |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Kalimantan". Britannica. Iliwekwa mnamo 2008-02-26.
- ↑ "Central Kalimantan Province". archipelago fastfact. Iliwekwa mnamo 13 Oktoba 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Indonesia General Info". Geohive.com. Iliwekwa mnamo 2009-08-11.