Nothing Special   »   [go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Europa (mitholojia)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Europa na fahali, sanamu ya kufinyangwa, mnanmo mwaka 470 KK, Makumbusho ya Staatliche Antikensammlungen mjini Munich
Europa na fahali, picha ya ukutani katika nyumba ya Kiroma huko Pompeii, Italia (karne ya 1 BK)

Europa ni jina la mwanamke katika mitholojia ya Ugiriki. Alikumbukwa kama binti wa mfalme wa Finisia katika Asia ya Magharibi aliyetongozwa na mungu mkuu Zeus na kupelekwa naye hadi kisiwa cha Krete. Jina lake lilikuwa hivyo jina la bara la Europa yaani Ulaya.

Katika masimulizi ya Europa Zeus ni mungu mkuu anayezunguka muda wote duniani akitafuta mapenzi na mabinti mazuri wa kibinadamu lakini anahitaji kujificha kwa sababu Hera, mke wake na mungu mkuu wa kike wa Wagiriki alichukia tabia hii. Kwa hiyo Zeus alibadilisha umbo lake mara kwa mara.

Alipotaka kumkaribia Europa mzuri aliingia katika umbo la fahali mweupe. Alimwamuru mungu wa biashara na wezi Herme kupeleka kundi la ng'ombe kwenye ufuko ambako Eruopa alicheza na mabinti wenzake. Mabinti walianza kucheza na ng'ombe waliokuwa watulivu na Europa alimpanda fahali mweupe. Hapo fahali Zeus alikimbia naye akaingia baharini na kuvuka bahari yote hadi kisiwa cha Krete. Hapa alichukua tena umbo lake la kawaida na kuzaa naye wana watatu. Europa aliolewa baadaye na Asterios mfalme wa Krete na kuwa malkia yake. Huyu hakuzaa mweyewe bali alikubali wataoto wake.

Mwana mmoja wa Zeus na Europa alikuwa Monos na huyu aliendelea kuwa mfalme wa Krete baada ya Asterios.

Hadithi hii ilihifadhiwa mara ya kwanza katika Illiadi ya Homer. Hapo babake aliitwa Phoinix.[1]. Kwa kipana ilishikwa katika mkusanyiko ulioitwa "Bibliotheke ya Apollodorus" [2]

  1. Illiad,xiv,321-322
  2. Apollodorus, Kitabu 3, Mlango wa kwanza, tovuti ya Theoi Classical Texts Library , iliangaliwa Novemba 2017