Nothing Special   »   [go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Barakoa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Barakoa ya Kiafrika.

Barakoa (pia: barkoa) ni kitambaa au kinyago kinachovaliwa usoni au kichwani chenye tundu kwenye macho, pua na mdomo linalotumiwa kukinga uso.

Kuna barakoa za kiutamaduni na barakoa za kinga.

Mfano mmoja wa barakoa za kiutamaduni ni Barakoa ya Sirige ya Wadogon wa Mali.

Pia ni nguo ya wanawake wa Kiislamu ambayo wanaivaa kwenye mapaji ya nyuso zao pamoja na buibui, ijulikanayo kama "burqa".

Kamusi ya Kiswahili Sanifu (1981) inaifafanua hivi : "kipande cha kitambaa kinachovaliwa na baadhi ya wanawake kutoka paji la uso mpaka mdomoni."

Na katika kamusi ya Frederick Johnson (1939) imeelezwa kwamba neno "barakoa" linatokana na Kiarabu برقع: "... kind of mask or veil covering the face down to the mouth, all but the eyes. Formerly worn in public by Muhammadan women, generally of the upper class, now rarely worn. As a rule the buibui is worn."

Barakoa za kinga zinavaliwa kwa shughuli mbalimbali, zikilenga kuzuia au kupunguza athira hatari za vumbi, gesi, hewa chafu au viini vya ugonjwa. Tangu kutokea kwa ugonjwa wa corona matumizi yake yameongezeka sana katika nchi nyingi za Dunia.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Barakoa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.