Nothing Special   »   [go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Bahari ya Shamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Bahari Nyekundu)
Eneo la Bahari ya Shamu ("Red Sea")

Bahari ya Shamu (kwa Kiingereza Red Sea; kwa Kiarabu البحر الأحمر Baḥr al-Aḥmar, al-Baḥru l-’Aḥmar; kwa Kiebrania ים סוף Yam Suf; kwa Kitigrinya ቀይሕ ባሕሪ QeyH baHri) ni ghuba kubwa ya Bahari ya Hindi. Jina la kihistoria katika lugha ya Kigiriki lilikuwa Bahari ya Eritrea (ερυθρά θάλασσα, erythrá thálassa).

Kaskazini kuna rasi ya Sinai pamoja ghuba ndogo za Aqaba na Suez; pia kwa sasa imeunganika na Mediteranea kwa njia ya Mfereji wa Suez. Kusini Bahari ya Shamu imeunganika na Bahari Hindi kwa njia ya mlango wa bahari wa Bab el Mandeb.

Ghuba yote ina urefu wa takriban kilomita 2000; upana wake ni kati ya km 300 na 20 tu kwenye Bab el Mandeb. Eneo lake ni km² 450,000.

Vilindi vyake vinaelekea hadi mita 2500 chini ya uwiano wa bahari. Vilindi hivyo ni sehemu ya Bonde la Ufa.

Halijoto ya maji ni kati ya 21-25 °C.

Nchi za kando

[hariri | hariri chanzo]

Nchi zinazopakana na Bahari ya Shamu ni: