Nothing Special   »   [go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Antwerpen

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mji wa Antwerpen

Antwerpen (Kifaransa Anvers) ni mji wa bandari katika kaskazini ya Ubelgiji mwenye wakazi 460,000. Ni mji mkubwa wa jimbo la Flandria.

Mji umeenea kando la mto Schelde unaoingia katika Bahari ya Kaskazini. Mdomo wake ni mpana wa kuruhusu meli kubwa kuingia ndani na ni mahali pa bandari ya Antwerpen ambayo ni bandari kubwa ya pili katika Ulaya ina nafasi ya 17 kati ya mabandari makubwa duniani.

Lugha ya wakazi wa Antwerpen ni Kiholanzi kwa lahaja ya Flandria. Kihistoria imekuwa mji wa Wakatoliki tangu 1585 ambako Waprotestanti walifukuzwa mjini. Kuna jumuiya muhimu ya Wayahudi waliofika kama wakimbizi kutoka Hispania na Ureno wakati wa karne ya 16. Wayahudi wamekuwa uti wa mgongo wa biashara ya almasi wakafanya Antwerpen kuwa kitovu cha biashara hii duniani. Wakati wa mwisho wa karne ya 20 Waturuki na Wamoroko walifika kama wafanyakazi walioleta dini ya Uislamu.

Kati ya wakazi mashuhuri wa Antwerpen alikuwa mchoraji wa karne ya 17 Peter Paul Rubens.

Makala hii kuhusu maeneo ya Ubelgiji bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Antwerpen kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.