Nothing Special   »   [go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Ceri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Ceri (Cerium)
Gramu 1.5 za seri safi iliyofunga ndani ya arigoni
Gramu 1.5 za seri safi iliyofunga ndani ya arigoni
Jina la Elementi
Ceri (Cerium)
Alama Ce
Namba atomia 58
Mfululizo safu Lanthanidi
Uzani atomia 140.116
Valensi 2, 8, 18, 19, 9, 2
Densiti 6.77 g/cm³
Ugumu (Mohs) 2.5
Kiwango cha kuyeyuka °K 1068
Kiwango cha kuchemka °K 3716
Asilimia za ganda la dunia ppm 66
Hali maada mango
Mengineyo nururifu

Seri ni elementi ya kimetali yenye alama ya Ce na namba atomia 58, maana yake kiini cha seri kina protoni 58 ndani yake. Uzani atomia ni 140.12. Ndani ya jedwali la elementi imepangwa kati ya lanthanidi.

Seri ni metali yenye rangi ya kijivu. Kwa joto la kawaida inapatikana katika hali mango. Si haba, duniani kuna ceri zaidi kuliko stani au risasi.

Ugunduzi

[hariri | hariri chanzo]

Ceri ilipatikana kwa mara ya kwanza nchini Uswidi mnamo mwaka 1803 na wataalamu Berzelius, wakati huhuo pia na Hisinger na Klaproth huko Ujerumani. Kwa sababu ni tendanaji sana, haikusafishwa hadi mwaka 1875. Ceri ilipewa jina la sayari kibete Ceres iliyotambuliwa miaka miwili kabla ya elementi mnamo 1801.

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Cerium haitumiwi mara nyingi kama metali kwani ina utendanaji wa haraka na hewa. Matumizi yake ya kawaida ni kama 'jiwe la kiberiti' kwa sababu hutoa kwa urahisi cheche inapopigwa na metali nyingine. Ceri hutumiwa pia katika aloi kwa sababu mara nyingi hufanya aloi kuwa ngumu zaidi. Ceri pia hutumiwa katika vioo maalum, kauri na oveni za kujisafisha.

Ceri ina isotopi nyingi. Nne kati yake hupatikana kiasili, nyingine ni sintetiki yaani zinazalishwa kwenye maabara.

  • Ceri-136 ambayo ina protoni 58 na neutroni 78 kwenye kiini chake, ni nururifu
  • Ceri-138 ambayo ina protoni 58 na neutroni 80, ni thabiti
  • Ceri-140 ambayo ina protoni 58 na neutroni 82, ni thabiti
  • Ceri-142 ambayo ina protoni 58 na neutroni 84, ni nururifu.
  • Ceri-140 (% 88.5 ya ceri yote) na Ce-142 (% 11.1) ni isotopi zinazotokea zaidi. Uzani atomia wa 140.12 ni wastani ya isotopi zote za ceri.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ceri kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.