Nothing Special   »   [go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Haramia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Uharamia)
Bendera ya kihistoria ya maharamia Wazungu kwenye Atlantiki

Haramia ni jambazi anayefanya mambo yake kwenye gimba la maji, hasa baharini.

Kufuatana na Mkataba wa Umoja wa Mataifa juu ya sheria za bahari uharamia ni matendo yoyote ya jinai yanayotekelezwa baharini na mabaharia au maabiria wa meli binafsi dhidi ya meli nyingine au dhidi ya watu na mali ndani yake.

Kisheria matendo ya aina hii dhidi ya ndege, mizigo au maabiria wake huitwa pia uharamia.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Katika historia maharamia wamejulikana tangu habari za kwanza juu ya usafiri kwenye bahari. Kati ya habari za kwanza ni zile kuhusu maharamia kwenye Mediteranea mnamo karne ya 13 KK.

Julius Caesar alipokuwa kijana alikamatwa na maharamia akaachiwa nao baada ya malipo ya fidia kubwa, lakini baadaye akarudi akalipiza kisasi na kuwaua maharamia.

Siku hizi eneo lenye uharamia mbaya ni Indonesia, lakini ni hasa maharamia wa Somalia walioonekana sana katika habari tangu mwaka 2008.

Wakati mwingine maharamia walitawala pia maeneo ya bandari walipokuwa na kimbilio chao kama dola-mji. Mfano mashuhuri wa madola hayo madogo ilikuwa jamhuri ya Bou Regreg katika Moroko ya leo wakati wa karne za 17-19.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]