Nothing Special   »   [go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Panya-mawe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Panya-mawe
Panya-mawe wa Namakwa (Aethonys namaquensis)
Panya-mawe wa Namakwa (Aethonys namaquensis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wanyama wagugunaji)
Familia ya juu: Muroidea (Wanyama kama panya)
Familia: Muridae (Wanyama walio na mnasaba na vipanya)

Nusufamilia: Murinae
Jenasi: Aethomys
Thomas, 1915
Ngazi za chini

Spishi 11:

Panya-mawe ni wanyama wagugunaji wa jenasi Aethomys katika nusufamilia Murinae ya familia Muridae. Huishi katika maeneo yenye mawe na miamba.

Msambazo

[hariri | hariri chanzo]

Panya-mawe wanatokea Afrika ya Mashariki na ya Kusini na spishi moja huko Kameruni na Nijeria. Spishi tatu tu hupatikana katika Afrika ya Mashariki: panya-mawe mwekundu, panya-mawe wa Hinde na Panya-mawe wa Kaiser.

Panya-mawe huonekana sana kama panya wa kawaida, kama panya kahawia, lakini pua yao ni nzito zaidi. Wana urefu wa sm 10-18 wenye mkia wa sm 12-20. Wana uzito kati ya g 50 na 110. Manyoya yao ni rangi fulani ya kahawia na pengine yenye kiasi cha nyekundu. Sehemu zao za chini ni nyeupe au kijivu iliyofifia.

Panya hao hukiakia kwa kawaida wakati wa usiku na hula mimea. Hujilisha kwa mchanganyiko wa dutu ya mimea iliyo na uwiano mkubwa wa mbegu. Hadi 10% ya lishe yao ni wadudu.