Nothing Special   »   [go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Jubilei

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jubilei (pia: Jubilii) ni sherehe maalumu za kuadhimisha tukio muhimu katika maisha ya mtu, shirika, asasi na kadhalika ambayo hufanyika kila baada ya kipindi fulani kama vile baada ya miaka ishirini (20), ishirini na tano (25) tangu kufunga ndoa au kuanzishwa kwa shirika fulani.

Jubilei ina mizizi yake katika Biblia. Torati ya Musa inaagiza kwa taifa la Israeli mwaka wa pekee kila baada ya miaka 50 (Mambo ya Walawi 25:10-13)

Jina linatokana na lugha ya Kiebrania ambapo neno "Yobel" linamaanisha aina ya tarumbeta (pembe ya kondoo dume) iliyotumika kuutangaza mwaka huo ambapo ulikuwa hasa na lengo la kupunguza tofauti za utajiri katika jamii, kuweka huru watumwa na kupumzisha ardhi.

Kuanzia mwaka 1300 Kanisa Katoliki limefufua kwa namna fulani adhimisho la namna hiyo (Mwaka mtakatifu), ambao urahisishe toba, msamaha wa dhambi na wa madeni na upatanisho kwa jumla kati ya binadamu na Mungu na kati ya watu wenyewe kwe wenyewe.

Adhimisho hilo katika Ukristo linamtegemea Yesu Kristo ambaye katika sinagogi la Nazareti aliutangaza "mwaka wa Bwana uliokubalika" (Injili ya Luka 4:16-21) uliotabiriwa na Isaya (61:1-2).

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jubilei kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.