Nothing Special   »   [go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Filipina Duchesne

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Roza Filipina.

Roza Filipina Duchesne, R.S.C.J. (29 Agosti 176918 Novemba 1852) alikuwa bikira wa Ufaransa, kati ya watawa wa kwanza katika shirika la Moyo Mtakatifu wa Yesu lililoanzishwa na Magdalena Sofia Barat [1]

Wakati wa Mapinduzi ya Ufaransa alikuwa ameshakusanya jumuia kuhudumia maskini akaiunganisha na shirika hilo[2].

Baadaye alitumwa Amerika, alipoanzisha shule nyingi na tawi la shirika hilo nchini Marekani[3].

Papa Pius XII alimtangaza mwenye heri tarehe 12 Mei 1940, halafu Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu tarehe 3 Julai 1988.

Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka kwenye tarehe ya kifo chake[4].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Baunard, Louis (1892). Histoire de la vénérable mère Madeleine-Sophie Barat : fondatrice de la Société du Sacré-Cur de Jésus. Paris: Ch. Poussielgue.
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/90437
  3. "A Brief History of the Society of the Sacred Heart", Society of the Sacred Heart, United States – Canada
  4. Martyrologium Romanum
  • Catherine M. Mooney, Philippine Duchesne: A Woman with the Poor (NY: Paulist Press, 1999; rpt. Wipf & Stock, 2007)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.