Umoja wa Afrika
Umoja wa Afrika (UA) (kwa Kiingereza: African Union (AU); Kifaransa: Union Africaine (UA); Kihispania: Unión Africana (UA) ; Kireno: União Africana (UA) ) [1] ni muunganiko wa nchi 55 za Afrika ulioanzishwa mnamo Julai 2002.
Umoja huu unaendeleza kazi za Umoja wa Muungano wa Afrika (kwa Kiingereza: Organisation of African Union - OAU) uliokuwepo 1963 hadi 2002.
Nia ya umoja huu ni kujenga muundo na mfumo wa kisiasa, wa kiuchumi, na wa kijamii ili kufikia wakati ambapo bara la Afrika litakuwa na bunge moja, benki moja, jeshi moja, raisi mmoja, sarafu moja, n.k.
Dhumuni kubwa la umoja huu ni kuunganisha nguvu za mataifa ya Afrika ili kuweza kutatua matatizo yanayokabili bara hili kama vile vita, njaa, Ukimwi, n.k.
Nchi wanachama
Umoja wa Afrika ina nchi wanachama 55, yaani nchi zote za bara la Afrika (baada ya kurudi kwa Moroko, iliyokuwa imejiondoa mwaka 1985 kwa sababu UA ilitambua Sahara ya Magharibi kuwa nchi huru wakati Moroko inadai ni eneo la majimbo yake ya kusini). [2][3]
Mkutano wa kwanza wa Bunge la Umoja wa Afrika ulifanyika mwaka 2004 huko Afrika Kusini.
Mikutano mikuu ya UA
- Durban (Afrika Kusini): 9-11 Julai 2002.
- Maputo (Msumbiji): 10-11 Julai 2003.
- Sirte (Libya), mkutano wa dharura: Februari 2004.
- Addis Ababa (Ethiopia): 6-8 Julai 2004.
- Abuja (Nigeria): 24-31 Januari 2005.
- Sirte (Libya): 28 Jun. - 5 Julai 2005.
- Khartoum (Sudan): 16-24 Januari 2006.
Viongozi
- Thabo Mbeki 9 Julai 2002 10 Julai 2003 Afrika Kusini
- Joaquim Chissano 10 Julai 2003 6 Julai 2004 Msumbiji
- Olusegun Obasanjo 6 Julai 2004 24 Januari 2006 Nigeria
- Denis Sassou-Nguesso 24 Januari 2006 24 Januari 2007 Jamhuri ya Kongo
- John Kufuor 30 Januari 2007 31 Januari 2008 Ghana
- Jakaya Kikwete 31 Januari 2008 2 Februari 2009 Tanzania
- Muammar al-Gaddafi 2 Februari 2009 31 Januari 2010 Libya
- Bingu wa Mutharika 31 Januari 2010 31 Januari 2011 Malawi
- Teodoro Obiang Nguema Mbasogo 31 Januari 2011 29 Januari 2012 Guinea ya Ikweta
- Yayi Boni 29 Januari 2012 27 Januari 2013 Benin
- Hailemariam Desalegn 27 Januari 2013 30 Januari 2014 Ethiopia
- Mohamed Ould Abdel Aziz 30 Januari 2014 30 Januari 2015 Mauritania
- Robert Mugabe 30 Januari 2015 30 Januari 2016 Zimbabwe
- Idriss Déby 30 Januari 2016 30 Januari 2017 Chad
- Alpha Condé 30 Januari 2017 28 Januari 2018 Guinea
- Paul Kagame 28 Januari 2018 10 Februari 2019 Rwanda
- Abdel Fattah el-Sisi 10 Februari 2019 10 Februari 2020 Misri
- Cyril Ramaphosa 10 Februari 2020 madarakani Afrika Kusini
Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya UA ni N. Dlamini-Zuma.
Spika wa Bunge la Umoja wa Afrika ni Roger Nkodo Dang.
Tanbihi
- ↑ "Official Languages AU "Art. 11 AU" Protocol on amendments to the constitutive act of the African Union" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2014-06-30. Iliwekwa mnamo 2014-09-06.
- ↑ [1]
- ↑ "Morocco seeks to rejoin African Union after 32 years". BBC News. 18 July 2016. Retrieved 18 July 2016.
Viungo vya nje
- (Kiingereza) Tovuti ya Umoja wa Afrika Archived 15 Aprili 2012 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |